WANAMUZIKI MWANZA WAZINDUA MAADHIMISHO KIMATAIFA YA SIKU YA MUZIKI DUNIANI KWA KUTEMBELEA KISIWA CHA SAANANE ISLAND

Wanamuziki jijini Mwanza wakiwa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane Island wakati walipo kitembelea ikiwa ni moja ya shughuli ya Maadhimisho ya Siku ya  Kimataifa  ya Muziki Duniani kwa   lengo la kutangaza utalii wa ndani.

Wanamuziki hao wakiwa katika hifadhi hiyo.
Wanamuziki jijini Mwanza wakiwa kwenye boti maalumu wakati wa kutembelea kisiwa hicho.

Utalii ndani hifadhi hiyo ukiendelea.
Wanamuziki jijini Mwanza wakiwa katika picha mbalimbali kwenye hifadhi hiyo.
Utalii ndani hifadhi hiyo ukiendelea.
 


Dotto Mwaibale  


WANAMUZIKI jijini Mwanza wamezindua  Maadhimisho ya Kimataifa  ya Siku ya Muziki Duniani kwa kutembelea Kisiwa cha Saanane Island lengo likiwa ni kutangaza utalii wa ndani.

Wanamuziki hao walifanya safari hiyo ya kitalii katika kisiwa hicho jana ikiwa ni moja ya shughuli kuelekea Maadhimisho ya Siku hiyo ambayo kilele chake kitakuwa ni Oktoba 1, 2021 Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Stella Joel alisema  Wanamuziki wa kada mbalimbali katika baadhi ya mikoa wameshiriki kuzindua maadhimisho hayo katika maeneo yao kwa kuhamasisha shughuli mbalimbali za  maendeleo.

Alisema kwa Dar es salaam Wanamuziki hao walikutana Makumbusho ya Taifa iliyopo Posta ambapo walikuwa na jumbe mbalimbali za Kuhamasisha maendeleo ya shughuli za kijamii pamoja na kuutangaza muziki.

Joel alisema kwa upande wa Arusha Wanamuziki walikutana katika Makumbusho ya Kihistoria ya Taifa na kupata historia mbalimbali ikiwemo ya kuanzishwa kwa Azimio la Arusha.

Alisema na kwa Mkoa wa Mwanza  walitembelea kisiwa hicho cha Saanane Island.

Joel alitumia nafasi hiyo kumshukuru sana Mhifadhi wa Kisiwa hicho cha Saanane Island Kamanda Eva Mwangomo kwa kuupa heshima Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) ambao umeandaa maadhimisho hayo kwa kutoa fursa ya kutembelea kisiwa hicho kwa lengo la kukitangaza  na kufanya ziara hiyo ya utalii wa ndani kujionea vivutio vya utalii wa nchi yetu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments