FEDHA ZA TOZO YA MIAMALA YA SIMU KUJENGA MADARASA ZAIDI YA 500 | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 2, 2021

FEDHA ZA TOZO YA MIAMALA YA SIMU KUJENGA MADARASA ZAIDI YA 500

  Malunde       Thursday, September 2, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan amesema fedha zitakazokusanywa katika tozo za miamala ya simu mwezi huu wa Septemba na Oktoba mwaka huu, zitatumika kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya 500 nchini na kuboresha miundombinu ya elimu.Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Tegeta mkoani Dar es Salaam aliposalimiana na Wakazi wa eneo hilo, akiwa njiani kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani kurekodi filamu yenye lengo la kuitangaza Tanzania.

Amesema hatua hiyo itawawezesha Wanafunzi wanaotaka kuanza shule au kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2022 kukuta vyumba vya madarasa viko tayari pamoja na miundombinu mingine ikiwa imeboreshwa.

Rais Samia Suluhu Hassan amewaeleza Wakazi hao wa Tegeta na Watanzania wote kuwa tozo zitaendelea kuwepo, kwa sababu zinasaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amefafanua kuwa, katika kipindi cha miezi miwili pekee tangu Serikali ilipoanza kutoza tozo katika miamala ya simu imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 60, ambazo zitatumika kujenga vituo vya afya 220 katika maeneo mbalimbali nchiniUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post