RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA KANSELA WA UJERUMANI, ANGELA MERKEL | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, September 2, 2021

RAIS SAMIA AZUNGUMZA NA KANSELA WA UJERUMANI, ANGELA MERKEL

  Malunde       Thursday, September 2, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Katika mazungumzo hayo, Merkel amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushika hatamu za Urais nchini Tanzania na kumpa pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. 

Pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kupambana na UVIKO 19 na kuahidi kuunga mkono jitahada hizo kwa kutoa msaada wa chanjo za kukabiliana na ugonjwa huo.

Aidha, Merkel amesema mwezi Oktoba mwaka huu Serikali yake itaanzisha majadiliano na Serikali ya Tanzania kuhusu maeneo ambayo Serikali ya Shirikisho la Ujerumani inaweza kusaidia kutokana na athari za UVIKO 19.

Pia, Merkel amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambapo ameahidi kuwashawishi wafanyabiashara wa Ujerumani na watalii kutembelea na kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake Rais Samia Suluhu Hassan amemshukuru Merkel kwa ushirikiano wake na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Amempongeza kwa kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa ni kiongozi wa kisiasa mwanamke aliyeongoza muda mrefu ndani ya Chama chake cha CDU na ndani ya Jumuiya ya Ulaya.

Aidha, Merkel amesema mwezi Oktoba mwaka huu Serikali yake itaanzisha majadiliano na Serikali ya Tanzania kuhusu maeneo ambayo Serikali ya Shirikisho la Ujerumani inaweza kusaidia kutokana na athari za UVIKO 19.

Pia, Merkel amempongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini ambapo ameahidi kuwashawishi wafanyabiashara wa Ujerumani na watalii kutembelea na kuwekeza nchini Tanzania.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Merkel kwa ushirikiano wake na Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo. Amempongeza kwa kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa ni kiongozi wa kisiasa mwanamke aliyeongoza muda mrefu ndani ya Chama chake cha CDU na ndani ya Jumuiya ya Ulaya.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post