WALIMU WATANO, MLINZI WAKAMATWA KWA KUVUJISHA MTIHANI WA DARASA LA SABA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Fortunatus Musilimu

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watuhumiwa 6 kwa kuhusika na njama za kuvujisha mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika hivi karibu wakiwemo walimu watano na mlinzi mmoja waliokuwa wakisimamia mtihani katika Shule ya Msingi Kambara wilayani Mvomero.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro (SACP) Fortunatus Musilimu, amesema watuhumiwa hao ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambara Juliana Thomas, Msimamizi Mkuu wa Mtihani Antonia Pastory, Mwalimu Doma Sekondari, Mtoto Francis, Mwalimu Shule ya Msingi Kinda, Mwalimu Dorine James wa Shule ya Msingi Madizini, Mwalimu Habibu Hango na Mlinzi wa mtihani kituo hicho Mohammed Bajuka.

Aidha, Kamanda Musilimu amesema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wengine watano kwa kupatikana na nyara za serikali yakiwemo meno matatu ya Tembo yenye uzito wa kilogramu 23.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments