MIZENGO PINDA AZINDUA UVCCM GREEN CUP KITAIFA SHINYANGA MJINI...ANG'OA VIGOGO WA UPINZANI

 

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akipiga Penati kuzindua Rasmi mashindano ya michezo ya UVCCM GREEN CUP, katika uwanja wa Michezo CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, amezindua rasmi mashindano ya michezo ya Umoja wa Vijana (UVCCM GREEN CUP).

Uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja wa michezo CCM Kambarage Mjini Shinyanga, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama ,Serikali na wadau wa michezo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, amesema amefurahishwa na umoja huo wa vijana UVCCM, kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo ni muhimu katika kuimarisha afya.

“Mashindano haya ni jambo jema sana katika kuunganisha nguvu za vijana na kuimarisha afya, na kuishinda Corona ni kufanya mazoezi,”amesema Waziri Mkuu Mstaafu Pinda.

Aidha, amekitaka Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Shinyanga ,kuwa ili kuenzi neno Green (kijani), ni kuwatumia vijana wa umoja huo UVCCM, katika kuhakikisha wanapanda miti ya kutosha na kuifanya Shinyanga kuwa ya kijani.

Pia  aliupongeza Mkoa wa Shinyanga, kwa kufanya mazoezi kila Jumamosi, na kuomba hiyo iwe kama Sera ya mkoa huo, ili kuimarisha afya za watumishi pamoja na wananchi.

Katika hatua nyingine aliutaka mkoa wa Shinyanga kufanya Tathimini ya maendeleo ya kiuchumi pamoja na kufanya mkutano mkubwa, ambapo mkoa una fursa nyingi za uwekezaji kutokana na wingi wa malighafi, ikiwemo Mifugo, Pamba, na zao la Tumbaku.

Awali Katibu wa  UVCCM Mkoa wa Shinyanga Muhsin Zikatim, akisoma taarifa ya umoja huo kwa wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, alisema mashindano hayo ya michezo mbali na kuimarisha afya. pia yatakuza utalii wa ndani, ambapo vijana wa UVCCM Shinyanga Oktoba 3 watakwenda Zanzibar kwenye mashindano hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, alisema mashindano hayo ya UVCCM GREE CUP ni ya kitaifa, lakini yamezinduliwa mkoani Shinyanga, huku akiahidi suala la upandaji miti litakuwa endelevu ili kuifanya Shinyanga kuwa ya kijani.

Aidha katika uzinduzi huo wa UVCCM GREEN CUP, Vigogo watatu kutoka vyama vya upinzani walihamia Chama cha Mapinduzi CCM, akiwemo Renatus Nzemo, aliyekuwa Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti, Charles Shigino, aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi NCCR Mageuzi, pamoja na Emmanuel Aluta, aliyekuwa Afisa Utawala na Fedha kutoka TLP.


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akizungumza kwenye uzinduzi wa Michezo UVCCM GREEN CUP katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga. Picha na Marco Marco Maduhu

Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira , Mhe. Patrobas Katambi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akizungumza kwenye uzinduzi wa Michezo ya UVCCM GREEN CUP.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa UVCCM GREEN CUP.

Mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, akizungumza kwenye uzinduzi wa Michezo ya UVCCM GREEN CUP.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Muhsin Zikatim, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa UVCCM GREEN CUP.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (kulia) , akiteta jambo na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge, kwenye uzinduzi wa UVCCM GREEN CUP.

Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiwa kwenye uzinduzi huo wa UVCCM GREEN CUP.

Baadhi ya wananchi mkoani Shinyanga, wakishuhudia uzinduzi wa UVCCM GREEN CUP.

Awali Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akipiga Penati kuzindua Rasmi mashindano ya michezo ya UVCCM GREEN CUP, katika uwanja wa Michezo CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana na wachezaji kutoka Shinyanga kwenye uzinduzi wa UVCCM GREEN CUP.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akisalimiana na wachezaji kutoka Zanzibar kwenye uzinduzi wa UVCCM GREEN CUP.

Soka likisakatwa.

Soka likiendelea kusakatwa kati ya Mashabiki wa Timu ya Simba na Yanga Manispaa ya Shinyanga.

Mashabiki wa Simba Manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja, kabla ya kusakata Soka kwenye uzinduzi wa mashindano ya michezo ya UVCCM GREEN CUP.

Mashabiki wa Yanga Manispaa ya Shinyanga wakipiga picha ya pamoja, kabla ya kusakata Soka kwenye uzinduzi wa mashindano ya michezo ya UVCCM GREEN CUP.

Mashindano Mbio za Baiskeli yakiendelea.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akiwapokea wanachama watatu kutoka vyama vya upinzani na kujiunga CCM, kushoto ni Charles Shigino aliyekuwa Katibu wa Siasa na Uenezi kutoka NCCR Mageuzi, akifuatiwa na Emmanuel Aluta aliyekuwa Afisa utawala na fedha kutoka TLP, pamoja na aliyekuwa Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti Renatus Nzemo.

Waziri Mkuu Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akipanda Mti nje ya uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga mara baada ya kumaliza kuzindua mashindano ya michezo UVCCM GREEN CUP, katikati ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Patrobas Katambi, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati.

Mwenyekiti wa Chama Chama Chamapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa naye akipanda Mti nje ya uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga ,mara baada ya kumalizika uzinduzi wa UVCCM GREEN CUP.

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akipiga picha ya pamoja na viongozi wa CCM, Serikali na baadhi ya wabunge mkoani Shinyanga, akiwemo Ahmed Salum wa Jimbo la Solwa mwenye shati jeupe na Patrobas Katambi Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini aliyechuchumaa katikati.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments