WAHANDISI NCHINI WATAKIWA KUENDELEA KUJISAJILI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, September 5, 2021

WAHANDISI NCHINI WATAKIWA KUENDELEA KUJISAJILI

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya  Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
Msajili wa Bodi ya Wahandisi Patric Barozi,akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya wahandisi, Prof. Ninatubu Lema,akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,(hayupo pichani) wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya  Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki mara baada ya kufunga  maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya  Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga  maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya  Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
.......................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imewataka wahandisi wote nchini kuendelea kujisajili chini ya Bodi ya  usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) ili waweze kutambulika kitaifa na kimataifa  .
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini ambapo zaidi ya  Wahandisi 3000 walihudhuria  huku Wahandisi 630 wakila kiapo.
Mhandisi Sanga amesema kuwa kujisajili kwa wahandisi ni takwa la kisheria hivyo mlango uko wazi kwa kila mhandisi kujisajili huku akihimiza kwa wahitimu fani ya uhandisi kutoka vyuo mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo.
''kufanya hivyo itasaidia zaidi wahandisi kuaminika kitaifa na kimataifa zaidi pamoja na kuepusha watu wanaofanya kazi ya uhandisi kutekeleza miradi ya miundombinu licha ya kuwa hawana vigezo hali ambayo husababisha miradi kutekelezwa kwa kiwango cha chini''amesema Mhandisi Sanga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wahandisi, Prof. Ninatubu Lema, amesema zaidi ya watu  800 wamefuatilia kwa njia ya mtandao hivyo idadi ya watu wote waliofuatilia ikiwa  ni zaidi ya 3700  ikivuka lengo ambapo matarajio ilikuwa ni watu 3200.
Naye Msajili wa Bodi ya Wahandisi Patric Barozi, amesema kuwa siku tatu kulihusishwa mijadala ya kitaaluma,Maonesho ya Ubunifu,Sayansi na Teknolojia huku pia Makampuni 61 yakishiriki.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages