VYAMA 16 VYACHUKUA FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA USHETU

NEC Habari, Ushetu- Shinyanga
Vyama 16 vya siasa vimejitokeza kuchukua fomu za uteuzi kugombea kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ushetu Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 Oktoba mwaka 2021.

Vyama vilivyojitokeza kuchukua fomu za uteuzi hadi kufikia tarehe 18 Septemba mwaka 2021 saa 10:00 jioni ni Chama cha DP, Chama cha CHAUMMA, NRA, ADC, AAFP, Sauti ya Umma (SAU),

Vyama vingine vilivyochukua fomu ni Cha cha ADA TADEA, UPDP, TLP, Demokrasia Makini, UMD, NLD, UDP, CCK, CCM na Chama cha ACT Wazalendo.

NEC Habari imeshuhudia baadhi ya wagombea wakichukua fomu za uteuzi huku kikuwepo na ushindani kati ya wanawake na wanaume ambapo kati ya vyama 16 vilivyochukua fomu, vyama nane (8) vimewakilishwa na wanawake.

Vyama vilivyoteua wawakilishi wanawake kuchukua fomu za uteuzi ni Chama cha ADC, AAFP, SAU, ADA-TADEA, UPDP, UMD, NLD na Chama cha CCK.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ushetu Bw. Linno Pius Mwageni amesema fomu za uteuzi kwa wagombea wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo zimeanza kutolewa tarehe 13 hadi tarehe 19 kesho Jumalipi itakuwa ni siku ya Uteuzi wa wagombea.

Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi  wa Jimbo la Ushetu Godfrey Samwel Lwambura amewataka wagombea hao kuhakikisha wanajaza fumo za uteuzi kwa usahihi na siku watakaporejesha fomu hizo watajaza Fomu Namba 10 ya kuheshimu Maadili ya Uchaguzi.

Kwa mujibu wa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ushetu iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 20 Septemba, 2021 hadi tarehe 8 Oktoba, 2021 na Siku ya Kupiga Kura itakua tarehe 9 Oktoba mwaka 2021.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments