TGNP : TUNAMPONGEZA DKT. STERGOMENA LAWRANCE TAX KWA KUTEULIWA KUWA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Monday, September 13, 2021

TGNP : TUNAMPONGEZA DKT. STERGOMENA LAWRANCE TAX KWA KUTEULIWA KUWA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 13 Septemba, 2021.

PONGEZI KWA DKT STERGOMENA LAWRANCE TAX KWA KUTEULIWA KUWA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA.

Kwa niaba ya wanachama, bodi ya wakurugenzi na wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), kwa furaha kubwa sana tunapenda kumpongeza Mhe. Dkt. Stergomena Lawrance Tax kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Hii imetengeneza kestoria ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kushika nafasi hiyo. Kwa upande wa Afrika Mashariki, Dkt. Tax amekuwa mwanamke wa tatu kuwa Waziri wa Ulinzi baada ya kuwa na Mawaziri wa Ulinzi wanawake nchini Kenya, ambao ni Raychelle Omamo (May 2013- Januari 2020) na Monica Juma (Jan 2020 hadi sasa). Hatua hii ni kubwa sana katika historia ya harakati za ukombozi wa wanawake kimapinduzi nchini na Afrika kwa ujumla.  


Dkt. Tax hivi karibuni alimaliza muda wake akihudumu kama katibu mtendaji (mwanamke wa kwanza) katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na pia amewahi kuwa katibu mkuu katika wizara mbali mbali nchini Tanzania, katika wizara za Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Viwanda, Biashara na Masoko na Fedha na Mipango.  

 

Ni matarajio yetu na watanzania kwa ujumla kuwa kutokana na uzoefu wake Dkt. Tax katika nafasi yake ya Uwaziri wa Ulinzi na Ujenzi wa Taifa ataendelea kusimamia haki, amani, usalama, uzalendo na kutetea wanyonge hasa wanawake na makundi yaliyopembezoni dhidi ya dhuluma za kijinsia ili kudumisha amani na usalama na kulileletea taifa maendeleo endelevu na jumuishi yenye kuzingatia usawa wa kijinsia.  
Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

No comments:

Post a Comment

Pages