Tanzia : MWANDISHI WA AZAM TV NICOLAUS NGAIZA AFARIKI DUNIA - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Monday, September 6, 2021

Tanzia : MWANDISHI WA AZAM TV NICOLAUS NGAIZA AFARIKI DUNIA

Muonekano wa gari baada ya ajali
Nicolaus Ngaiza enzi za uhai wake
Mwandishi wa habari wa Azam Media mkoa wa Kagera Nicolaus Ngaiza amefariki dunia usiku huu Septemba 5,2021 baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka wilaya ya Biharamulo walipokwenda kikazi kupata ajali katika eneo la Gwanseli wilayani Muleba.

Katika ajali hiyo pia mwandishi wa habari wa Clouds Media Group Benson Eustace, alikuwemo na amejeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera wodi namba nne akiendelea kupatiwa matibabu.

Ajali hiyo imetokea wakati wakiwa njiani kurudi Bukoba.
R.I.P Nicolaus NgaizaDownload/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

No comments:

Post a Comment

Pages