TAIFA STARS YAIBAMIZA MADAGASCAR MABAO 3-2 | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 7, 2021

TAIFA STARS YAIBAMIZA MADAGASCAR MABAO 3-2

  sayarinews.co.tz       Tuesday, September 7, 2021

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika mchezo wa kufuzu kushiriki kombe la Dunia mwakani baada ya kuinyuka timu ya taifa ya Madagascar mabao 3-2 katiika dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Dakika ya kwanza tu mpira unavyoanza Taifa Stars ilifanikiwa kupata penati baada ya Simon Msuva kuchezewa rafu mbaya na kipa wa madagascar akijaribu kuokoa shambulizi la kushtukiza.

Penati ilipiga na Erasto nyoni na kufanya ubao uusomeke 1-0 Taifa Stars kuongoza.

Dakika ya 26 Novatus Dismas alifanikiwa kufunga bao zuri na kufanya Taifa Stars kuongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 36 Rakotohoharimala kupachika bao na baadae Fontaine kuisawazishia timu yake ya taifa na kwenda mapumziko matokeo yakiwa 2-2.

Kipindi cha pili timu zote zilikuwa zinahitaji ushindi katika mchezo huo ambapo walikuwa wanafanya mashambulizi ya kushtukiza kwa timu zote mbili.

Feisal Salumu aliibuka shujaa dakika ya 52 baadaa ya kupachika bao zuri akipokea pasi murua kutoka kwa mshambuliaji Mbwana Samata na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post