RAIS MWINYI ATUMA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA JAJI WA MAHAKAMA KUU ZANZIBARI HAJI OMARI HAJI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 11, 2021

RAIS MWINYI ATUMA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA JAJI WA MAHAKAMA KUU ZANZIBARI HAJI OMARI HAJI

  Malunde       Saturday, September 11, 2021

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi
**
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha Jaji Haji Omar Haji, Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Kifo cha Jaji Haji Omar Haji kimetokea leo katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa kesho Shakani, Wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja mnamo saa saba za mchana.

Katika salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Jaji Haji Omar Haji.

Aidha, kupitia salamu hizo za rambirambi, Rais Dk. Mwinyi alimuomba Mwenyezi Mungu kuwapa moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hichi kigumu cha msiba, familia, marafiki, ndugu pamoja na wafanyakazi na viongozi wote wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Salamu hizo ziliendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kumpa rehma na kumjaalia makaazi mema peponi. Amin.


Marehemu Jaji Haji Omar Haji aliteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar mnamo Februari 01, 2021 na kuapishwa mnamo Februari 08, 2021.


Sambamba na hayo, mnamo Agosti 16, 2021 marehemu Jaji Haji Omar Haji aliteuliwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Jaji Omar Othman Makungu kuwa Jaji Mkaazi Pemba.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post