NAIBU WAZIRI DKT MABULA AHIMIZA UHAKIKI KWA WAMILIKI WA ARDHI

 Na Munir Shemweta, BUKOMBE
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wamiliki wa wa ardhi kujitokeza katika zoezi la uhakiki linaloendelea katika ofisi zote za ardhi nchini.



Alisema, uamuzi wa wizara yake kufanya uhakiki wa wamiliki wa ardhi ni kutaka kuwatambua wamiliki kwa majina yanayosomeka kwenye vitambulisho vya NIDA.

‘’Tumachotaka ni kukutambua kama wewe ni mmiliki wa kiwanja kilichopo Bukombe au Sumbawanga kwa majina yale yale yanayosomeka katika kitambulisho cha NIDA’’ alisema Dkt Mabula.

Akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Bukombe  mkoani Geita tarehe 15 Sept 2021 Naibu Waziri Mabula alisema, hatua ya kufanya uhakiki itaisaidia Wizara ya Ardhi kama serikali kupata kumbukumbu nzuri za watanzania wanaomiliki ardhi na kusisitiza kuwa hakuna ukomo kwenye umiliki na mtu mmoja anaweza kumiliki viwanja zaidi ya ishirini.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, kumekuwa na sintofahamu kuhusiana na zoezi hilo la uhakiki ambao baadhi ya watu wanasita na kufikiri serikali inataka kuwanyang’anya viwanja ambapo alisisitiza kuwa, lengo ni kutaka kuwatambua wamiliki kwa majina yao.  na kubainisha kwamba kama kuna majina ya watoto basi yatatenganishwa  vya kwako na vya watoto

‘’Tunachotaka ni kuondoa wamiliki bandia ambao hata ukiwatafuta huwapati kwa kuwa jina aliloandika siyo la kwake, na kama kuna majina ya watoto basi yatenganishwe na ya kwako’’ Dkt Mabula

Aidha,  alisema kuwa uhakiki unaoendelea utasadia pia kwenye masuala mazima ya mirathi hasa pale mmiliki atakapofariki huku akiwa hakutumia majina yake kwenye umiliki wa viwanja vyake na kuongeza kuwa, ikitokea mmiliki amefarikia basi familia yake ijue rasilimali zake.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Said Nkumba alimshukuru Naibu Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula kwa kuitembelea wilaya hiyo na kukutana na viongozi pamoja na watumishi wa sekta ya ardhi ambapo alisema ujio wake utasiadia sana wilaya yake kujipanga katika masuala mazima ya ardhi hasa kwenyematumizi bora ya ardhi.

Nkumba pia aliunga mkono wazo la Naibu Waziri wa Ardhi kutaka halmashauri ya wilaya ya Bukombe kuangalia namna ya kuwakopesha viwanja watumishi wa serikali waliopo kwenye wilaya hiyo ili waweze kujikwamua katika masuala ya makazi.

‘’Kama huwezi kukopa basi hata kukopa kiwanja? Na nafikiri suala la kukopa viwanja ni jambo jema na ni vizuri tukaanza na watumishi kwa kuwa unalipa kidogokidogo na huwezi kujua unaweza kukaa hapa Bukombe mpaka unastaafu na sisi tunaona ni jambo jema’’ alisema Mkumba.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments