MBUNGE WA JIMBO LA NAMTUMBO ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA GARI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, September 19, 2021

MBUNGE WA JIMBO LA NAMTUMBO ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA GARIMbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa amepata ajali katika eneo la Nalasi wilayani Tunduru akiwa kwenye ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme ambaye ana ziara leo huko Namtumbo, mkoani Ruvuma. Mbunge huyo alikuwa watu wengine watatu kwenye gari na wote wametoka salama.( Picha na CCM Makao Makuu)
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa akiwa amenusurika kwenye ajali ya gari lake alilokuwa akilitumia katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Christine Mdeme.
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe. Vita Kawawa akizungumza na Bw. Nasoro Hassan Dereva wa CCM Makao Mkuu mara baada ya kunusurika kwenye ajali ya gari lake alilokuwa akilitumia katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndugu Christine Mdeme.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages