PINDA ATAKA CCM USHINDI WA KISHINDO JIMBO LA USHETU, KATA YA NDEMBEZI

 


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Shinyanga.


Na Marco Maduhu, Shinyanga

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, amekitaka Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoani Shinyanga, kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ushetu wilayani Kahama, na Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Alibainisha hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Shinyanga, alipowasili mkoani humo kwa ajili ya kuzindua rasmi mashindano ya michezo ya Umoja wa Vijana wa Chama hicho UVCCM GREEN CUP Kitaifa, katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Alisema Jimbo la Ushetu lilikuwa chini ya Marehemu Elias Kwandikwa, na Kata hiyo ya Ndembezi ilikuwa chini ya Marehemu David Nkulila, ambao wote walitoka Chama Cha Mapinduzi CCM, na walifariki Agosti mwaka huu siku tofauti, hivyo ni vyema kuwaenzi kwa kuwapatia viongozi wanaotokana na CCM.

“Katika uchaguzi mdogo wa wa Jimbo la Ushetu na Kata ya Ndembezi sina shaka tutashinda, na ili kuwaenzi viongozi hawa waliotangulia mbele ya haki, lazima tushinde kwa Kishindo, na nina kuomba Emmanuel Charahani ambaye umepitishwa na chama kugombea Jimbo la Ushetu, ujinyenyekeze kwa wapiga kura ili upate kura nyingi,”alisema Pinda.

Pia alikitaka Chama hicho kujiimarisha zaidi kwenye mashina, zikiwemo jumuiya za vijana, wazazi, na wanawake ili kukijenga chama, na wakifanikiwa kwenye hilo hakuna uchaguzi wowote watakaoshindwa, zikiwamo chaguzi zijazo wa Serikali za Mitaa 2024, na uchaguzi Mkuu 2025.

Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa, alimhakikishia Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, kuwa katika uchaguzi huo mdogo Jimbo la Ushetu na Kata ya Ndembezi watahakikisha wanapata ushindi wa kishindo,

Aidha katika Jimbo hilo la Ushetu lilikuwa chini ya Marehemu Elias Kwandikwa, ambaye pia alikuwa Waziri wa ulinzi, na katika Kata ya Ndembezi, ilikuwa chini ya David Nkulila ambaye alikuwa Meya wa Manispaa ya Shinyanga, ambapo tayari Tume ya Taifa (NEC) imeshatangaza uchaguzi mdogo kwenye majimbo yote pamoja na kata.


Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, akizungumza na Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Shinyanga.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akizungumza kwneye kikao hicho.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga Muhsin Zikatim, akisoma taarifa ya UVCCM kwenye kikao hicho.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa.

Wajumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Na Marco Maduhu- Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments