MAAFISA 21 WAKAMATWA KUHUSIANA NA JARIBIO LA MAPINDUZI SUDAN | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 22, 2021

MAAFISA 21 WAKAMATWA KUHUSIANA NA JARIBIO LA MAPINDUZI SUDAN

  Malunde       Wednesday, September 22, 2021


 Jeshi la Sudan limetoa taarifa likisema kwamba maafisa 21 na wanajeshi kadhaa wamekamatwa kuhusiana na jaribio la mapinduzi lililotokea jana asubuhi na msako unaendelea kuwakamata wengine waliobakia waliohusika na tukio hilo. 

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa jeshi ambaye ni mshauri wa masuala ya habari, Brigedia Jenerali Altahir Abu Haja, jeshi limeyadhibiti tena maeneo yote yaliyokuwa yamekamatwa wakati wa jaribio hilo. 

Aidha serikali ya mpito ya nchi hiyo imesema wanajeshi na raia waliohusishwa na jaribio hilo wanafungamanishwa na utawala ulioondolewa wa kiongozi wa muda mrefu, aliyeongoza kwa mkono wa chuma, Omar al-Bashir. 

Waziri Mkuu Abdalla Hamdok amesema jaribio hilo ni njama za hivi karibuni za kuchochea mgogoro wa kitaifa, akigusia mgawanyiko mkubwa uliopo Sudan wakati ikielekea kwenye demokrasia. 

Akihutubia kupitia Televisheni amesema waliopanga njama hiyo walifanya maandalizi ya kina ambayo yamejionesha kupitia mapungufu ya kiusalama yaliyoonekana mijini, kufungwa kwa barabara, bandari na uchochezi uliokuwa ukiendelezwa dhidi ya serikali ya kiraia.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post