TAARIFA YA MKUTANO WA MWAKA WA MASHIRIKA YA KISERIKALI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, September 22, 2021

TAARIFA YA MKUTANO WA MWAKA WA MASHIRIKA YA KISERIKALI

  Malunde       Wednesday, September 22, 2021
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini (NaCONGO) imeandaa Mkutano wa Mwaka wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuanzia tarehe 29-30 Septemba, 2021.

Mkutano huu utafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ukiwa na kauli mbiu isemayo: "Kuimarisha Mchango wa Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa".

Mgeni Rasmi katika Mkutano huu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanaalikwa kushiriki Mkutano huu kwa kujiandikisha kupitia tovuti ya www.nacongo.or.tz au piga namba +255 689 489554 au 0737569583 na 0737569584 kuthibitisha ushiriki wako.

Ujumbe huu umetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa ufadhili wa Shirika la Legal Services Facility.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post