JWT YAIPONGEZA SERIKALI KUWAONDOA MACHINGA MBELE YA MADUKA YA WAFANYABIASHARA

 

Na Magrethy Katengu -Dar es salaam

Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) imepongeza serikali kwa kuagiza Wamachinga kote nchini waondolewe mbele ya maduka ya wafanyabiashara walio rasmi wanaofuta taratibu za kuendesha shughuli zao za kibiashara.

Pombezi hizo amezitoa karibu mkuu wa jumiya ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) Abdallah Mwinyi ambapo amesema miaka michache iliyopita ulijitokeza mpangilio holela wa kufanya biashara popote kwa muda mrefu Hali ambayo ilifilisi wafanyabiasha wengi walio rasmi hadi wengine kuamua kutumia njia mbadala ya kufanya Biashara kwa kuwatumia hao hao machinga kuuza bidhaa zao

"Huu ni ukombozi mpya Kwa wafanyabiashara  Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa ujumla kwa kuagiza Wamachinga wote waondoke mbele ya maduka na makusanyo ya Kodi kwa taifa kwani tunatambua kuna wafanyabiashara walitumia kitambulisho cha mmachinga kama kichaka cha kukwepa kulipa kodi",alisema Mwinyi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mahusiano jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Stephen Chamle ameiomba serikali kufanya utafiti wa kutosha katika masoko yote kumbaini machinga kwa kuwawekea utaratibu namba ya kufanya biashara ili kuepusha migogoro kwani wote wanategemeana.

Hata hivyo jumuiya hiyo ya wafanyabiashara wameiyomba serikali kushirikishwa kwa kutoa maoni yao katika uwekezaji  Mradi mkubwa unaotarajiwa kufanyika Ubungo Kwa ujenzi wa kituo kikubwa cha Biashara kinachotarajiwa kuwa na maduka zaidi ya elfu tatu(3000).

Aidha Jumuiya hiyo imesema ushauri wao kabla ya Mradi huo kufanyika ni vyema kongamano kubwa lifanyike la uhuru wa maoni kwa wadau na waagizaji bidhaa kutoka nje ya nchi ili kuepusha watanzania kuwa watumwa wa biashara kwenye soko la ndani

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments