EWURA Yatangaza Bei Mpya za Mafuta ....Bei ya Petrol, Dizeli Yapanda

 Bei ya mafuta itapanda kuanzia leo kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dodoma na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), katika bandari ya Dar es Salaam bei ya petroli imeongezeka kwa shilingi 84, dizeli shilingi 29 na mafuta ya taa bei imeongezeka kwa shilingi 18.

Katika bandari ya Tanga bei ya petroli imeongezeka kwa shilingi 53, dizeli shilingi 14 na ya mafuta ya taa itabaki kama ilivyokuwa.

EWURA imesema katika bandari ya Mtwara petroli imeongezeka shilingi 108 na dizeli shilingi 46,

Taarifa hiyo ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji imesema bei ya mafuta katika mikoa mingine itategemea na wanachukulia wapi mafuta hayo kati ya bandari hizo, lakini bei ni elekezi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments