DAKTARI ATUPWA JELA KWA KUMDUNGA MKEWE SINDANO YA MAPEPO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, September 27, 2021

DAKTARI ATUPWA JELA KWA KUMDUNGA MKEWE SINDANO YA MAPEPO

  Malunde       Monday, September 27, 2021DAKTARI mmoja nchini Uingereza ambaye ni raia wa Misri, Hossam Metwally amehukumiwa kwenda jela miaka 14 baada ya kukutwa na hatia ya kumdunga mke wake sumu akiwa katika harakati za ‘kumuondoa mapepo’ yaliyokuwa yakimsumbua.

Hossam mwenye umri wa miaka 34, alipewa adhabu hiyo baada ya kumdunga mke wake Wilson sindano ya sumu aina ya Nicortin kwa lazima akidai anamtoa mashetani nyumbani kwao katika eneo la Grimsby.

Kufuatia ushahidi uliotolewa katika Mahakama ya Sheffield, Metwally alidaiwa kumshutumu mke wake kuwa na ‘majini ndani ya mwili wake.

Daktari huyo alipatikana na makosa nane ikiwemo kujaribu kumuua mke wake, ulaghai na pia kutazama picha za utupu baada ya kunaswa na kamera za siri alizoziweka katika ndani ya kliniki yake ya kibinafsi.

Metwally alikamatwa baada ya Wilson kupatikana akiwa mahututi na kupoteza fahamu mnamo Julai 4, 2019 na kulazimka kulazwa.

Kufuatia uchunguzi uliofanywa na polisi, ilibainika kuwa kiwango kikubwa cha sumu za nircotics, zikiwemo zile za aina ya ketamine, propofol na fentanyl zilitumika.

Hata hivyo, jambo la kushangaza zaidi ni kwamba daktari huyo bingwa wa upasuaji, hakuonyesha kujutia kitendo hicho alipokuwa akijitetea kortini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post