RAIS SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA 76 WA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA,NEW YORK..AGUSA CHANJO NA KASI YA UVIKO-19


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Jijini New York Nchini Marekani leo Septemba 23,2021

Rais Samia ameuomba Umoja wa Mataifa kuondoa hati miliki kwenye uzalishaji wa chanjo ya Uviko-19 ili mataifa mengi yaweze kuizalisha na kuitoa kwa wananchi wake  ili kuhakikisha kila Taifa linapambana na ugonjwa huo kwa kuwa usambazaji wake umekuwa wa taratibu kuliko mabadiliko ya kirusi chenyewe.

"Ombi letu ni kwamba hati miliki ya kutengeneza chanjo ya Uviko-19 itolewe kwa nchi zinazoendelea ili tuweze kupambana na janga hili hatari, hii sio tu hatua ya muhimu ya kumaliza janga hili lakini pia ni jambo sahihi litakalosaidia kuokoa ulimwengu mzima",amesema.

"Wakati chanjo ya Uviko-19 ilipokuwa ikifanyiwa utafiti ulimwenguni na baadaye kutengenezwa wengi tulikuwa na matumaini kwamba hii itakuwa na maana kubwa kwetu sote, tumekuja kugundua kwamba kirusi hiki kinasambaa haraka zaidi kuliko utengenezwaji na usambazaji wa chanjo", amesema Rais Samia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments