BABA AKAMATWA TUHUMA ZA KUBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 6



Jeshi la polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi wa kata ya Dutwa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka sita mbaye ni mtoto wake wa kambo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu, Richard Abwao alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kijiji cha Majengo, kata ya Dutwa wilaya ya Bariadi.

Abwao alisema mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Nduru Ndazi (49) anadaiwa kumnajisi mtoto huyo wa mkewe kwa tamaa ya kimapenzi.

Alisema mtuhumiwa huyo yuko mahabusu akisubiri kufikishwa mahakamani. Alitoa wito kwa wananchi kuacha vitendo vya ukatili na kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo hivyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Bariadi, Lilian Mishita alisema mtoto huyo baada ya kufikishwa hospitali na kufanyiwa vipimo katika hospitali ya wilaya ya Dutwa ilibainika kuwa ni kweli mtoto alifanyiwa kitendo hicho, tena inaonesha si mara moja.

Lilian pia aliomba jamii na asasi mbalimbali za kiraia kujitokeza kutoa elimu juu ya athari ya vitendo vya ubakaji kwa watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments