WIZARA YA MIFUGO YAANZA KUBAINI WAFUGAJI WALIOSHINDA KESI MAHAKAMANI | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, September 18, 2021

WIZARA YA MIFUGO YAANZA KUBAINI WAFUGAJI WALIOSHINDA KESI MAHAKAMANI

  Malunde       Saturday, September 18, 2021
Waziri wa Mifugo Mashimba Ndaki akizungumza na wafugaji.
**
Na Costantine Mathias Meatu
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi imeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa la kuitaka kuwatambua wafugaji wote walioshinda kesi zao mahakamani  za mifugo lakini hadi sasa hawajaweza kurejeshewa mifugo yao.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mifugo Mashimba Ndaki kwa nyakati tofauti mkoani Simiyu  katika kijiji cha  Longalambogo wilaya ya Itilima na kijiji cha Mwalilo wilaya ya Meatu wakati akizungumza na wafugaji wa maeneo hayo.

Amesema kuwa wanachokifanya kwa sasa ni kupita katika maeneo yote ambayo wafugaji walikuwa na migogoro na maeneo ya hifadhi za wanyama na mifugo yao kutaifishwa lakini wakawa wameshinda kesi mahakamani ila mifugo yao hawajarejeshewa hadi sasa.

Amesema kuwa kitendo cha kuwadhulumu wafugaji mifugo yao wakati wamepewa haki na vyombo vya sheria hakikubaliki hata kidogo.

Hivyo amewaagiza Wakuu wa wilaya za Itilima na Meatu kuhakikisha wanapeleka orodha ya wafugaji hao pamoja na vielelezo vyao vya kushinda kesi ili aweze kuiwasilisha kwa Waziri Mkuu ambaye naye ataipeleka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maamuzi.

Aidha ameshangazwa na baadhi ya maafisa mifugo katika wilaya kuwageuza wafugaji vitega uchumi vyao kwa kushiriki vitendo vya kuwadhulumu kwa kisingizio kuwa mifugo iliyotakiwa kurejeshwa kwa wafugaji wa wilaya ya Itilima ipatayo 280 imekwisha kufa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post