JAMAA ALIYEKUTWA NA DAMU YENYE RANGI NYEUPE AZUA GUMZO


Köhler anafanya kazi katika hospitali ya Chuo kikuu cha Cologne, nchini Ujerumani, ambapo mgonjwa alikuja akiwa anasumbuliwa na kichefuchefu , akitapika na maumivu ya kichwa.

Zaidi ya hayo, hali yake ya kumakinika ilikuwa inafifia.

Mgonjwa huyo mwanaume aliyekuwa na umri wa miaka 39 alikuwa anaumwa ugonjwa wa kisukari, lakini katika siku zilizotangulia alikuwa ameacha kumeza dawa zake mfululizo.

Kulingana na ripoti kuhusu kisa hiki, iliyochapishwa wiki hii katika jarida la masuala ya tiba - Annals of Internal Medicine , mwanaume huyo alikuwa amepelekwa kwenye kitengo cha dharura, ambako vipimo vilionesha kuwa damu yake ilikuwa na imepatwa na hali ya damu yake kuwa nzito kiasi cha kushindwa kuzunguka mwilini inayofahamika kama " hyperviscosity syndrome kutokana na viwango vya juu kupindukia vya mafuta -Triglycerides ."
Mgonjwa alikuwa na viwango vya juu vya mafuta katika damu yake

Triglycerides ni aina ya mafuta ya mwilini yatokanayo na vyakula tunavyokula kama vile siagi, na mafuta mengine tunayotumia kupikia vyakula, ingawa viwango vyake vya juu kutokana na sababu nyingine, kama vile, matatizo ya maumbile tunayorithi, unene wa kupindukia, baadhi ya dawa, unywaji wa pombe kupindukia na uvutaji wa sigara.

Tiba mbadala

Katika hali kama hii, madaktari hutumia mashine ya kukamua mafuta kutoka kwa damu na hivyo kupunguza uzito wake.

Hatahivyo hali ya mwanaume huyo ilikuwa ni ya kupindukia kiasi kwamba vichujio vya kuchuja mafuta vilikwama kwenye mafuta kwa sababu ya kuzibana na kuziba tena.

Iliwabidi madaktari wachukue hatua haraka ya kuondoa mafuta ya ziada, kurejesha rangi ya damu na hivyo kurejesha hali ya mgonjwa kuwa thabiti.

"Ilibidi tutafute mbinu mbadala ya matibabu ," Dokta Köhlera aliambia BBC . "Hata njia za kihistoria za kushusha viwango vya juu vya mafuta mwilini."

Lishe duni inaweza kusababisha maradhi ya kisukari.

Alipoona mchakati wa kawaida wa matibabu umeshindwa kupata ufanisi , Köhler na timu yake ya madaktari waliamua kufanya tiba inayoitwa phlebotomy, ambayo ni ya kuvuta damu yake yote mwilini na kumuwekea damu kutoka kwa mtu mwingine.

"Hatukuwa na la kufanya jingine," anasema Köhler. "Tulihitaji kumleta mgonjwa katika hali ambayo matibabu ya kawaida ya kuondoa mafuta kutoka kwenye damu ungewezekana tena."

Mbinu hii ilifanikiwa kwao, na wakaweza kushusha viwango vya mafuta kwenye damu.

"Kwa uelewa wetu, hili ni tukio la kwanza baya zaidi la mgonjwa kuwa na mafuta ya kupindukia kwenye damu kuwahi kushuhudiwa ambalo lilihitaji kufanyiwa mchakato wa kuvuta damu yake yote mwilini na kumpatia damu ya mtu mwingine ili kunusuru mgonjwa baada ya matibabu ya kawaida kutokuwa na ufanisi," anasema Köhler.

Damu ya maziwa
Mojawapo ya mambo yaliyowashangaza madaktari zaidi ilikuwa ni rangi ya damu ya mgonjwa.
Madaktari walilazimika kuondoa mafuta kwenye damu

"Mwanzoni rangi ilikuwa imepauka kuliko rangi ya kawaida inayopatikana kwenye mishipa," anasema Köhler. "Ilikuwa zaidi kama rangi ya misipa ya ateri lakini ilikuwa nyeupe yenye mng'aro."

"Baada ya kujichuja, damu nyeupe ikajitenga na damu ya kawaida, ambayo ilijichuja na kubakia chini ya chupa ya kukusanya damu)."

Köhler alikiambia kipindi cha Live Science kwamba damu iligeuka na kuchukua "rangi ya maziwa . "

Kulingana na dakatari huyo, mwanaume huyo sasa hana dalili za upungufu wa damu residual , na kwa sasa ameruhusiwa kutoka hospitalini na anapokea matibabu nje ya hospitali.

Kulingana na daktari Köhler , viwango vya juu vya mafuta katika damu ya mgonjwa vilisababishwa kushindwa kufany akazi kwa sukari ya mwili, unene wa kupindukia, lishe isiyofaa, na ugonjwa wa kisukari ambao haukutibiwa ipasavyo.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments