MKUTANO WA 18 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NCHI ZA AFRIKA 'AMCEN' WAFANYIKA


Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la umoja wa mataifa  - UNEP kanda ya Afrika Dokta Juliette Biao Koudenoukpo 

Rais wa AMCEN Waziri wa mazingira, Misitu na uvuvi wa Afrika Kusini  Bi Barbara Creecy.
**

Mkutano wa 18 wa baraza la mawaziri wa mazingira wa nchi za Afrika –AMCEN umefanyika leo tarehe 16 Septemba 2021 ukiwa umebeba kauli mbiu ya inayosema “Kulinda ustawi wa watu na kuhakikisha utunzaji endelevu wa mazingira Afrika”.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo kwa njia ya mtandao Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa  - UNEP kanda ya Afrika Dokta Juliette Biao Koudenoukpo amesema mawaziri wa mazingira kutoka nchi 54 za Afrika wanakutana kila baada ya miaka miwili au mitatu kujadili masuala yanayohusu mazingira katika nchi zao.

Dokta Koudenoukpo amesema mkutano wa AMCEN kwa kawaida unatanguliwa na  kikao cha wataalamu wa mazingira Afrika kilichofanyika tarehe 13 na 14 Septemba mwaka huu.

Dokta Koudenoukpo ameeleza kuwa kwa kuwa mkutano wa wakati huu umefanyika kukiwa na tatizo la ugonjwa wa CORONA duniani hiyo agenda zimegawanywa katika sehemu kuu mbili, ya kwanza ikiwa ni kushughulikia masuala ya haraka ya uratibu ya AMCEN ambapo ya pili ni kukubaliana kuahirisha yale masuala yanayohitaji mazungumzo hadi mwaka ujao wa 2022.  

Mkutano huo umewaleta pamoja wawakilishi wa nchi 54 za Afrika wanachama wa AMCEN pamoja na wadau mbalimbali kutoka kwenye wizara za nchi wanachama, mashirika binafsi, mashirika ya kijamii, wadau wa maendeleo na taasisi za umoja wa mataifa.

Mkutano wa mwaka huu umeongozwa na Rais wa AMCEN Waziri wa mazingira, Misitu na uvuvi wa Afrika Kusini  Bi Barbara Creecy.

AMCEN imeanziashwa mwaka 1985 kwa lengo la kukuza ushirikiano wa kikanda kati ya serikali za Afrika na washirika wao katika kushughulikia changamoto za mazingira zinazojitokeza.

Kupitia AMCEN serikali za nchi wanachama zimeimarisha sera za mazingira na kushirikiana na asasi za kiraia na sekta binafsi katika kuimarisha ulinzi na uhifadhi endelevu wa mazingira Afrika.

 

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post