Picha : WAZIRI BASHUNGWA AZINDUA REDIO MPYA 'GOLD FM' ...ATAKA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UENDANE NA WAJIBU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air' - Picha na Kadama Malunde

Na Projestus Binamungu WHUSN - Kahama
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye uhuru wa vyombo vya habari akisisitiza uhuru huo kwenda sambamba na wajibu.

Waziri Bashungwa ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Septemba 3, 2021 wakati akizindua Kituo cha Matangazo mmini Kahama mkoani Shinyanga kilichopewa jina la Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz chenye kauli mbiu ya 'Sauti ya dhahabu'.

Akizungumza katika mahojiano maalum mara baada ya uzinduzi wa kituo hicho Waziri Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hasaan inathamini na kuamini katika uhuru wa vyombo vya habari kupaza sauti za watanzania ili kuyafikia matamanio yao.

Waziri Bashungwa amesema “Serikali ya awamu ya sita kwa kuthamini uhuru wa vyombo vya habari inakusudia kuondoa asilimia 50 ya ada za tozo mbalimbali za leseni kwenye marekebisho ya kanuni za maudhui ya mtandaoni na maudhui ya utangazaji katika redio na televisheni”.

Ameongeza kuwa “Wamiliki wa mitandao ya kijamii kama YouTube ambayo maudhui yake siyo ya kihabari wataruhusiwa kupakia video zao mitandaoni bure, kama sehemu ya kuwawezesha kujitangaza na kujiingizia kipato zaidi”.

Akizungumzia uwekezaji huo Waziri Bashungwa amekaririwa akisema “Ninafurahi kuona uwekezaji wa namna hii unaenda sehemu husika (Kahama), na endapo mtahitaji kuanzisha television nawashauri mkiweza anzeni mapema na mkihitaji msaada tuambieni hiyo ndiyo kazi yetu” .

Katika hatua nyingine Waziri Bashungwa amezungumzia maendeleo ya mchakato wa kupata vazi la taifa amesema Serikali kupitia wizara yake inakusudia kuwakutanisha wabunifu wa mavazi wa hapa nchini na kuwapa fursa ya kubuni vazi litakalo shindanishwa na kupigiwa kura ili kupata mavazi kadhaa yatakayotumika kama mavazi rasmi ya kumtambulisha Mtanzania.

“Serikali iliona ni vyema iandae utaratibu ambao kupitia kwa wabunifu wa mavazi wenye wabuni na waseme kuwa hili linafaa kuwa vazi la taifa, na vazi hili siyo lazima liwe moja, yanaweza kuwa hata mawili n ahata matatu lakini yale ambayo yatashindanishwa na kushinda”, alisema Waziri Bashungwa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo aliwataka watangazaji na waandishi wa habari kuwa wabunifu zaidi ili kuitendea haki leseni ya utangazaji inayotolewa na mamlka hiyo kwa nia ya kuwawezesha watanzania kuhabarishwa kwa ubunifu zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Gold FM Bi. Neema Mghen ameiomba Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa kushirikiana na Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kuvijengea mazingira wezeshi vituo vichanga vya redio ili viendelee kuwa daraja la kuwasaidia wasanii wachanga kutimiza ndoto zao.

Uzinduzi wa kituo hicho cha redio cha Gold FM kinaifanya wilaya ya Kahama kuwa na vituo Vinne vya redio huku kwa mkoa wa Shinyanga vikifika vituo vitano ambavyo ni redio Gold FM, Kahama FM, Divine FM, Huheso FM na Radio Faraja Fm.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na wafanyakazi wa Gold Fm. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Zoezi la Uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm likiendelea
Zoezi la Uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm likiendelea
Muonekano wa sehemu ya Jengo la Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akisaini Kitabu cha Wageni wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), Emmanuel Cherehani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akiingia katika chumba cha habari wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (wa pili kushoto) akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga, Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo ( wa kwanza kulia akifuatiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen (wa pili kulia) wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ndani ya chumba cha kutengenezea vipindi (Production Room)
Meneja wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Faraji Mfinanga (kulia) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa ndani ya chumba cha kutengenezea vipindi (Production Room)
Mtangazaji wa Vipindi vya Redio, Juma Athuman (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (aliyekaa kulia) ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'. Wa Kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo, Kushoto aliyekaa ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga, aliyesimama mwenye suti ya bluu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Mtangazaji wa Vipindi vya Redio, Juma Diwani (kulia) akimuuliza swali Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) wakati akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (kushoto) akizungumza Mubashara ndani ya chumba cha Kurushia Matangazo ' Studio On Air'
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Kulia ni Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wilaya ya Kahama, Emmanuel Cherehani na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati akizindua Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kahama Timoth Ndanya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Gold Fm
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Gold Fm
Wafanyakazi wa Gold Fm
Wafanyakazi wa Gold Fm
Mwenyekiti wa KACU,Emmanuel Cherehani akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm, Bi Neema Mghen akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa TCRA Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Zoezi la kukata keki likiendelea
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Matangazo cha Gold Fm kinachosikika kupitia masafa ya 88.7Mhz 'Sauti ya Dhahabu' kilichopo Mjini Kahama Mkoani Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments