MAPACHA WAFARIKI MAMA YAO MZAZI AKIWA BIZE FACEBOOK | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, September 21, 2021

MAPACHA WAFARIKI MAMA YAO MZAZI AKIWA BIZE FACEBOOK

  Malunde       Tuesday, September 21, 2021INASIKITISHA SANA! Matukio mengine ukimwambia mtu si rahihi kumuingia akilini, imagine mtu anapoteza watoto wake wapendwa tena mapacha eti kisa yuko live kwenye mitandao ya kijamii, like seriously?

Watoto wawili mapacha wamefariki dunia mara baada ya kuporomoka kutoka ghorofa ya kumi wakati mama yao akiwa amezama LIVE katika mtandao wa Facebook.

Mapacha hao ambao ni Moise Petrice wa kiume na Beatrice Petrice pacha wa kike wamekumbwa na umauti huo baada ya kudandia katika dirisha lililokuwa limeachwa wazi. Tukio hili limejitokeza katika jiji la Ploiesti nchini Romania.
Polisi wamethibitisha kwamba mama wa watoto hao hakugundua kama wanae wameporomoka na kufariki dunia hadi hapo aliposikia milio ya magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) huku kukiwa na mtu akibisha hodi mlangoni kwake.

Muda wote huo mpaka watoto wanafariki yeye alikuwa bize LIVE Facebook akiongea na wafuasi wanaomfuatilia katika ukurasa wake wa mtandao huo wa facebook.

Imeelezwa dhahiri kuwa wakati mama huyo Andreea Violeta Petrice aliposahau kufunga dirisha ambalo watoto hao walilitumia kucheza kwa kujaribu kutoka na ndipo walipodondoka na kupoteza maisha.

Mara tu baada ya kumfungulia mlango mtu yule ailyekuwa akibisha hodi alimpasha habari kuwa kulikuwa na watoto mapacha wamedondoka na kufariki dunia. Mama huyo kwa haraka alikwenda chumbani kwa watoto wake ili kujua kama ni wake na ndipo dhahiri alipogundua kuwa hawakuwa ndani na dirisha lilikuwa wazi.

Yaani uyu mama nadhani hatarudi tena kutumia mitandao ya kijamii na iwe mwisho kabisa, unawezaje kuacha watoto, kwanini asingeteremka nao alikokuwa anafanyia hiyo live, ama ilikuwa ni ya muhimu sana mpaka aache Mungu amtie nguvu.

Lakini watu inabidi tusi zubae sana hususa ni kwenye hii TikTok maana ndiyo nyingine inayopelekea watu puta na ndio maana India waliufuta maana waliona watu watawehuka sana.

Hata hivyo, hata kama mitandao tunaitumia kutuingizia pesa, yatupasa kuwa makini nayo ili isiweze kutufanyia hivi na kutufanya vituko kwenye jamii.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post