WANAUME WAONGOZA KUPATA CHANJO YA CORONA TANZANIA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, August 15, 2021

WANAUME WAONGOZA KUPATA CHANJO YA CORONA TANZANIA

  Malunde       Sunday, August 15, 2021

Jumla ya watu  207,391 wamepatiwa chanjo ya UVIKO - 19 nchini Tanzania kwa hiari iliyoanza kutolewa hivi karibuni katika vituo vya kutolea huduma zaidi ya 550 kwa Tanzania bara.

Katika taarifa kwa Umma leo 15 Agosti, juu ya maendeleo ya utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 kwa Wanananchi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kwa Katibu Mkuu (Afya), Prof. Abel Makubi amebainisha kuwa:

Tathimini ya zoezi la utoaji chanjo tangu Mikoa yote izindue tarehe 04/08/2021, inaonesha mpaka kufikia tarehe 14.08.2021, jumla ya walengwa 207,391 wamepatiwa chanjo hiyo kwa hiari, kati ya hao waliopatiwa chanjo hiyo, walengwa 121,002 ni wanaume ambao ni  sawa na asilimia 58 (58.3%) na Wanawake ni 86,389 sawa na asilimia 41 (41.7%).
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post