Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Monday, August 16, 2021

RAIS SAMIA AONDOKA NCHINI KUELEKEA MALAWI KUSHIRIKI MKUTANO WA 41 WA SADCRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hii leo Agosti 16, 2021 ameondoka Nchini kuelekea Nchini Malawi kwaajili ya kushiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika kuanzia tarehe 17-18 Agosti, 2021.Katika uwanja wa ndege wa Jijini Dodoma , Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesindikizwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages