KENYA NA TANZANIA ZAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO ZA CORONA


 Na. WAMJW, Nairobi.
Makatibu Wakuu wa Wizara za Afya pamoja na Wataalam wa Wizara hizo kuoka nchini Tanzania na Kenya wamekutana leo jijini Nairobi na kuweza kujadili changamoto zinazowakabili nchi hizo mbili ikiwemo ya UVIKO-19 kwa upande wa mipakani.

Prof. Abel Makubi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania amesema mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Afya jijini Nairobi ulikuwa na lengo la kutekeleza makubaliano yaliyofanyika kati ya Marais wa nchi hizo mbili walipokutana mwaka huu jijini hapa wa kuondoa changamoto za masuala ya Corona kwa upande wa kibiashara.

Amesema mkutano huo ambao ulitanguliwa na kikao cha awali cha wataalum wa sekta hiyo na baadae kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu hao waliweza kujadiliana masuala ya upimaji wa Corona baina ya nchi hizo mbili na kuweza kukubaliana ni namna gani ya kuondoa changamoto za ugonjwa huo.

“Tumekutana ili kuweza kuondoa changamoto za Corona ambazo Marais wetu Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na Mhe. Uhuru Kenyata walikutana na kuona yapo masuala yanayoleta changamoto hususan kwenye biashara kati ya Tanzania na Kenya na kuondoa mashirikiano katika mipaka yetu,hivyo kama wataalam tumekutana ili kuweza kuziondoa changamoto hizo na kuboresha mashirikiano”.

Prof. Makubi alitaja mambo waliyoyajadili ni pamoja na suala la kuhakikisha kwamba kunakuwa na mifumo inayoweza kuwasiliana katika upimaji kwa kuweza kuonekana kwa upande wa Tanzani na wakati huo huo kwa upande wa Kenya.

“Mfano kama mtu amepimwa ‘PCR’ basi aweze kusomwa na kuonekana pande zote mbili na mifumo yetu iweze kusoma kote na hiyo itaweza kusaidia kama nchi na wananchi wetu kuweza kufanya biashara vizuri” Aliongeza.

Aidha, kwa upande wa gharama za upimaji hususan kwa madereva wa magari makubwa alisema wamejadili na kutoa mapendekezo ambayo yatapekekwa kwenye kikao cha Mawaziri wa nchi hizo mbili, kikao ambacho kitakachofanyika siku ya Alhamisi na kuweza kutoa maamuzi ya mwisho.

Kwa upande wa mashirikiano katika kukabiliana na Corona kwa ujumla Prof. Makubi alisema wameweza kujadili masuala ya takwimu,chanjo pamoja na kubadilishana uzoefu baina ya nchi hizo mbili na mategemeo yao ni kwamba mapendekezo waliyoafikiana leo yataweza kuamliwa na kutolewa utekelezaji na Mawaziri hao ili shughuli za wananchi zisije kuathiriwa kwa uwepo wa Corona kwa maana ya shughuli za kikazi,familia na kibiashara.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kutoka Kenya Bi. Susan Mochache amesema kuwa mazungumzo kati ya wizara hizo mbili kuhusiana na ugonjwa wa Corona kama mazungumzo ya Marais wa nchi hizo mbili walivyokubaliana kushirikiana katika upande wa sekta ya afya hususan katika vita vya Corona wamejadili na kutoka na mapendekezo kadhaa.

Bi.Mochache alisema wamejadili kuweza kurahisisha biashara kati ya nchi hizo mbili ikiwemo biashara ya kupitisha mizigo tofauti ikiwemo chakula kutoka Tanzania kuingia Nchini Kenya na vile vile Kutoka nchini Kenya kuingia Tanzania.

“Tumekuwa na changamoto katika mipaka yetu kwasababu ya misimamno tofauti tuliyokuwa nayo baina ya nchi zetu hizi mbili lakini tumeweza kukubaliana vile tutawezesha uchumi na kibiashara kuendelea kuboreshwa na kuweza kuondoa miongozo na ‘protocol’ ile ambayo hazikuwa zinafaa kwa wanacnhi wa Kenya na Tanzania.

Alisema wameweza pia kuzungumza kuhusiana na mifumo ambayo inatumika baina ya nchi hizo mbili na kuweza kusaidi Serikali kwani awali kulikuwa na udanganyifu kwa madereva katika suala la upimaji.

Mkutano huu wa Makatibu Wakuu ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Afya Katika nchi mbili ambao unatarijiwa kufanyika keshokutwa jijini hapa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post