Breaking

Post Top Ad

Monday, August 23, 2021

WAFANYAKAZI WATANO WA TRA WAFARIKI KWENYE AJALI YA GARI


Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Land Cruiser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso wakati wakitekeleza majukumu yao.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe ACP Janeth Magomi amesema ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika eneo la Hanseketwa - Old Vwawa wilayani Mbozi, Songwe.

Kamanda Magomi amesema kwamba ajali hiyo imesababisha vifo vya wafanyakazi wanne wa TRA mkoa wa Mbeya na mmoja wa TRA Tunduma, ambapo wote walikuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya doria mipakani kwa lengo la kukomesha biashara ya magendo.

Taarifa za awali zinadai kuwa Watumishi hao walikuwa kazini, ambapo walikuwa wakitumia gari hiyo kufukuza gari nyingine iliyohisiwa kubeba bidhaa za magendo.

Miili ya marehemu hao wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Songwe..

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages