HAWA NDIYO WENYE SIFA YA KUFUNGISHA NDOA TANZANIA



Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi amesema viongozi wa dini ambao hawajasajiliwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini-RITA hawataruhusiwa kufungisha ndoa ya aina yoyote hadi watakapo jisajili na kupata kibali cha kufungisha ndoa.

Waziri Kabudi amesema endapo viongozi hao wa dini watafungisha ndoa bila ruhusa kutoka RITA ndoa hiyo haitatambulika na itakuwa batili.

Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika maadhimisho ya nne ya siku ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu barani Afrika yenye kauli mbiu isemayo uongozi kwa huduma muhimu kujenga mifumo imara ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu barani Afrika inayowezesha ubunifu, ushirikishwaji na ugatuzi katika utoaji huduma baada ya kipindi cha Uviko 19.

"Kwa mujibu wa sheria ya ndoa kila kiongozi wa dini anaruhusa ya kufungisha ndoa mpaka alete maombi RITA na asajiliwe na kuruhusiwa, kiongozi wa dini ambaye hajapata kusajiliwa na hajaruhusiwa na RITA kuwa msajili wa ndoa, ndoa anayoifunga kisheria ni batili" ameeleza Prof Kabudi

"Ni vizuri viongozi wa dini wapya wanapopatikana wanatakiwa kuwa na ruhusa ya kufungisha ndoa maombi ya kaenda rita na wakaingia kwenye tangazo la serikali kwamba hawa ndio waliopewa ruhusa yakufungisha ndoa" ameongeza Prof Kabudi

Prof. Kabudi amesema RITA inatazamia kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa usajili wa vyeti vya ndoa ambao utachangia kutoa takwimu na taarifa zote muhimu za ndoa huku akiitaka rita kuhakikisha mfumo huo unakamilika kwa wakati na kabla haujazinduliwa ikutane na wadau wote wa masuala ya ndoa ili kuwapa elimu.

Awali akizungumza kabla ya Waziri wa Katiba na Sheria, Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi wa Haki za Kisheria Lina Msanga amebainisha kwamba lengo la maadhimisho ya nne ya siku ya usajili wa matukio muhimu ya binadamu barani Afrika ni kuongeza mwamko na kasi ya wananchi kusajili matukio muhimu ya binadamu barani Afrika ya yakiwemo matukio ya vifo na ndoa.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments