JAMAA AMSHTAKI MKEWE KWA KUDANGANYA ANA MIMBA AKIFUNGA NGUO TUMBONI MIEZI 9 KISHA KUNUNUA MTOTO

Mwanaume mmoja aitwaye Westley Rono mwenye umri wa miaka 37 amemshtaki mke wake kwa kudanganya kwamba alikuwa mjamzito licha yeye kufahamu alikuwa tasa.

Wesley Rono kutoka Kuresoi Kusini Nakuru nchini Kenya alisema mke wake alimweleza Disemba 2020 kwamba alikuwa amepata mimba ya mtoto wao wa kwanza, alifurahishwa na habari hizo bila ya kujua zilikuwa porojo tupu.

Kwa mujibu wa taarifa za The Standard, Rono ambaye ni mfanyabiashara mkubwa Kuresoi, alisema aliamua kujibwaga kwenye mchezo huo wa paka na panya.

Rono alisema Patricia angegadhabishwa kila mara angejaribu kupapasa tumbo yake ambayo kila siku alikuwa akiijazilia nguo ili aonekane kuwa mjamzito.

" Niligundua kwamba mke wangu alikuwa akijifunga nguo kwenye tumbo yake na hangekubali nimguse, ningejaribu kumpapasa, angegadhabishwa na kuzua ugomvi, nilikuwa nagharamia malipo yake ya kwenda kliniki pia," Rono alisema.

Baada ya miezi tisa kukamilika, Patricia alimwambia mumewe kwamba anahitaji pesa za kununua mahitaji ya msingi ya mtoto na pia ya kulipia bili ya hospitali baada ya kujifungua.

Patricia aliondoka nyumban Agosti 8 akisema anaelekea hospitalini kujifungua na angemweleza kila tukio, kwa masikitikio yake, mwanamke huyo alimpigia simu na kumwambia kwamba alikuwa amejifungua mtoto wa kiume.

" Ujasiri wake kusema ukweli ulinishtua, sidhani kuna mwanamke anaweza kujifungua na saa chache kama kakika 30 hivi apande Matatu," Alisema Rono.

Rono aliongezea kwamba Patricia alienda nyumbani kwao ili aweze kupata nafuu kwanza, alirejea kwake siku chache baadaye na mtoto huyo ambaye kulingana na Rono alionekana kuwa wa miezi kama nne hivi.

Rono hakupata amani moyoni mwake, aliamua kupiga ripoti kwa polisi akishuku huenda mkewe alimununua mtoto huyo.

" Mke wangu alighushi kila kitu, alijaribu kila mbinu kunipumbaza, hapa kamwe siwezi nikamsamehea," Aliongezea Roho.

Patricia alikiri kumnunua mtoto huyo akisema kwamba alimpatia mlanguzi wa watoto mbegu za miti kama malipo.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments