WATUMISHI MAMLAKA YA MAJI MOSHI 'MUWSA' WATEMBELEA MTAMBO WA KUTIBU MAJITAKA SHINYANGA

 


Afisa Mauzo Msaidizi kutoka Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi MUWSA, Matha Urio ambaye pia ni Mkuu wa Msafara akiongoza baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo ya Maji Moshi, katika ziara ya kujifunza na kubadilisha uzoefu wa kazi kwa mamlaka ya maji Shinyanga SHUWASA.Na Marco Maduhu, Shinyanga

Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA), wametembelea mtambo wa kutibu Majitaka ( Faecal Sludge Treatment Plant) katika Manispaa ya Shinyanga na kuridhishwa namna ulivyotekelezwa kutoa huduma hiyo.
Mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV).

Mkuu wa msafara wa watumishi hao Matha Urio, ambaye pia ni Afisa Mauzo Msaidizi kutoka MUWSA, akizungumza leo mara baada ya kumaliza kutembelea eneo hilo la kutibu majitaka, ambapo alisema wamefurahishwa na hatua hiyo.

"Sisi ni baadhi ya watumishi kutoka Moshi MUWSA, ambapo tupo hapa mkoani Shinyanga kwa ziara ya siku mbili, tumekuja kujifunza na kuona wenzetu wa SHUWASA namna wanavyotoa huduma zao kwa wateja", alisema Urio.

"Katika mtambo wa kutibu majitaka ambao tumeutembelea leo, tumeona namna utakavyotoa huduma kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga na wananchi wa maeneo yaliyo karibu watanufaika kwenye shughuli za kilimo," aliongeza.

Kwa upande wake Mhandisi wa Usambazaji Maji kutoka SHUWASA, Uswege Mussa, akitoa maelezo kuhusu mtambo wa kutibu majitaka kwa watumishi wa MUWSA, alisema mradi huo umesaidia kuuweka mji wa Shinyanga katika mazingira safi.

Alisema tayari huduma ya majitaka imeanza kupelekwa katika eneo la kutibu majitaka na mengi ni maji kutoka majumbani hali inayofanya Manispaa ya Shinyanga kuwa na Usafi wa Mazingira ukilinganisha na awali huduma hiyo haikuwepo.


Afisa mauzo msaidizI kutoka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Moshi MUWSA, Matha Urio, ambaye pia ni Mkuu wa Msafara akiongoza baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Moshi, akielezea namna walivyoridhishwa na Mtambo wa kutibu Majitaka.

Mhandisi wa usambazaji maji kutoka SHUWASA, Uswege Mussa, akitoa maelezo kuhusu mtambo wa kutibu majitaka kwa watumishi wa MUWSA

Mhandisi wa usambazaji maji kutoka SHUWASA, Uswege Mussa, akiendeleaa kutoa maelezo kuhusu mtambo wa kutibu majitaka kwa watumishi wa MUWSA

Ziara ikiendelea kwenye Mtambo wa kutibu Majitaka.

Ziara ikiendelea kwenye Mtambo wa kutibu Majitaka.

Ziara ikiendelea kwenye Mtambo wa kutibu Majitaka.
Ziara ikiendelea kwenye Mtambo wa kutibu Majitaka.

Ziara ikiendelea kwenye Mtambo wa kutibu Majitaka.

Ziara ikiendelea kwenye Mtambo wa kutibu Majitaka.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga SHUWASA, wakipiga picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi MUWSA, mara baada ya kumaliza kutembelea Mtambo wa kutibu Majitaka ulipo Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Shinyanga SHUWASA, wakipiga picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Moshi MUWSA, mara baada ya kumaliza kutembelea Mtambo wa kutibu Majitaka ulipo Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu- Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post