MWANDISHI WA AYO TV AFARIKI KWA AJALI YA GARI

 Mwandishi wa Habari wa Ayo TV, Nellyson Grigery amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Agosti 18, 2021 katika eneo la Kibaha mkoani Pwani.

Taarifa ya Kifo cha mwandishi huyo imethibitishwa na mmiliki wa televisheni hiyo ya mtandaoni, Millard Ayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Leo imekua siku ngumu sana kwangu na AyoTV Team tumeondokewa na marafiki zetu wawili na mmoja ni mfanyakazi mwenzetu, mpigapicha wa AyoTV Kanda ya Ziwa, Nellyson Grigery,”ameandika Ayo.

“Mwingine ni rafiki yetu Mujitaba Yusuf waliekuwa wakisafiri pamoja kutoka Mwanza kuja Dar. Wamepata ajali Kibaha wakiwa watatu tunamshukuru Mungu mtu wa tatu ambaye ni Khamis Abdallah Mwandishi wa AyoTV Kanda ya Ziwa amejeruhiwa na sasa anaendelea vizuri,"ameongeza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments