WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MOROCCO


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Julai 12, 2021 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa wa Morocco Nasser Bourita na Waziri Mkuu wa Morocco Saad Dine El Otmani.

Katika Mzungumzo hayo Waziri Mkuu alizungumzia kuimarisha ushirikiano mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na Morocco ulioasisiwa na kujengwa na wasasisi wa nchi hizi mbili Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mfalme Mohammed V.

Sponsored: Je, Unatafuta Kazi Serikalini? Bofya Hapa

Waziri Mkuu alisisitiza umuhimu wa nchi hizi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Kilimo, Utalii, Nishati na Uvuvi.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar Leila Muhamed Mussa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments