MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA BILIONI 37.9 MKOANI TABORA


NA TIGANYA VINCENT
Jumla ya miradi mbalimbali ya Maendeleo 37 yenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 37.9 inatarajiwa kuzinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Tabora zinazoanza kesho.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake.

Alisema kwenye miradi hiyo Serikali kuu imechangia 35.7, Halmashauri zimechangia milioni 963  , wananchi wamechangia milioni 142.

Balozi Dkt. Batilda amesema ujumbe mkuu wa Mbio hizi Maalum za Mwenge wa Uhuru 2021 ni “TEHAMA ni msingi wa taifa endelevu; itumie kwa usahihi na uwajibikaji”

Amewaomba  wananchi wote wa Mkoa wetu wa Tabora kujitokeza na kushiriki mahali ambapo Mwenge wa Uhuru utapita na kushuhudia jitihada za Maendeleo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Balozi Dkt. Batilda amewakumbusha wakazi wa Mkoa wa Tabora  kuendelea kuchukua tahadhari kubwa kwa Ugonjwa wa COVID 19 katika maeneo na shughuli zote za Mwenge wa Uhuru na Vitakasa mikono(Sanitizer), kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments