HAWA NDIYO WANAFUNZI BORA 10 WALIOFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SAYANSI MATOKEO KIDATO CHA SITA 2021


Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa Kidato Cha Sita  mwaka 2021 pamoja na matokeo ya mtihani wa ualimu.

Bofya Hapa chini Kutazama

👉👉MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) 2021


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2021 na kutaja wanafunzi kumi bora waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi.

Akizungumza leo Jumamosi Julai 10, 2021 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amemtaja Perucy Astus Mussiba kutoka shule ya Canossa, Dar es Salaam kuwa kinara wa matokeo hayo, katika masomo ya sayansi mchepuo wa PCB.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Donard Rulers Mosile kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri (Arusha) kutoka PCB. Cretus Amos Mihayo kutoka Tabora Boys (Tabora) PCB akishika nafasi ya tatu akifuatiwa na Ismail Mtumwa kutoka Kibaha Sekondari(Pwani) PCM aliyeshika nafasi ya nne.

Nafasi ya tano imechukuliwa na Olais Julius Mollel kutoka Kisimiri (Arusha) PCM akifuatiwa na Geofrey Sanga aliyeshika nafasi ya sita kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM.

Anord Msanga kutoka Tabora Boys (Tabora) PCM akichukua nafasi ya saba Caroline Mpale amechukua nafasi ya nane kutoka Canossa Sekondari( Dar es Salaam) akichukua mchepuo wa PCM.

Nafasi ya tisa na kumi imechuukuliwa na wanafunzi kutoka Feza Boys (Dar es Salaam) PCM John Bugeraha aliyechukua nafasi ya tisa na Harry Mshana aliyechukuwa nafasi ya kumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments