WASANII MKOA MWANZA WAUNDA JUKWAA LAO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, July 10, 2021

WASANII MKOA MWANZA WAUNDA JUKWAA LAO

  Malunde       Saturday, July 10, 2021

Ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao katika sanaa, Wasanii wa Mkoa wa Mwanza leo wameamua kuanzisha Jukwaa la Wasanii Mkoa wa Mwanza ili kuwaleta pamoja katika sanaa.

Wakizungumza katika kikao cha leo Jumamosi Julai 10,2021 kilichopewa jina la Get Together, Wasanii hao wamekubaliana kwa kauli moja kuanzisha Jukwaa hilo ambalo litahusika na Kuratibu shughuli zote sanaa katika Mkoa wa Mwanza na mikoa ya Jirani.

Msanii Mkongwe wa Muziki wa Bongo Flava H Baba amesema ameona jitahada za Wasanii wa Mkoa wa Mwanza, huku akipongeza kwa Jukwaa hilo kuundwa maana litawaleta Wasanii wa sekta zote kutoka Mkoa wa Mwanza.

"Mwanza Wasanii Wote wanafanya vizuri ila shida iliyokuwepo ni matabaka na umimi ila kuanzia leo, tunaunda Jukwaa la Wasanii Mkoa wa Mwanza ili kuwaleta pamoja Wasanii wa aina zote ili kushirikiana katika mambo yote ya Sanaa na kijamii", amesema H Baba.

Naye Mdau Mwandamizi wa Sanaa Mkoa wa Mwanza William Bilunda ameomba pamoja na Jukwaa hilo kuratibu shughuli mbalimbali za sanaa ila pia Jukwaa lihusike kubuni Kampeni mbalimbali za kijamii pamoja na kuwapa kuwaongezea elimu ya sanaa wasanii wote.

Kwa Upande wake Katibu wa Wasanii wa Kuigiza Mkoa wa Mwanza Edward Kimbulu amesema Jukwaa hilo litaleta muunganiko wa Wasanii wa sanaa zote Mkoani Mwanza na kurahisisha Umoja na ushirikiano wa nyanja mbalimbali.

Jumla ya Wasanii zaidi ya hamsini  wameshiriki katika kikao hicho, Wasanii hao ni kutoka Sanaa ya Kuigiza, Kuimba, Kuchekesha, Kudensi na Wadau wa Sanaa kama Watangazaji, Madjs na Waandishi wa Habari kutoka Mkoa wa Mwanza.

Sambamba na hayo leo pia imeundwa Kamati ya Usimamizi, Mipango na Uratibu Ili kuliongoza Jukwaa hilo katika kutimiza matakwa ya kiserikali na kuandaa mikakati yake mikubwa waliyoipendekeza wasanii 
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post