MASHUHUDA WAELEZA TUKIO LA GIFT MUSHI ALIVYOPIGWA RISASI NA ALEX KAROSSO


Mashuhuda wameeleza kuwa Gift Mushi aliyepigwa risasi jana alikumbwa na tukio hilo, baada ya kumshauri Alex Korosso aache tabia ya kuwatishia watu kuwapiga risasi  wakati wakipata kinywaji.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea jana Julai 17,2021 katika baa ya New Lemax  iliyopo maeneo ya Sinza kwa Remmy

Mashuhuda wamesema siku ya tukio Korosso alifika kwenye baa hiyo aliyezoea  kunywa akiwatisha wenzake na kwamba anatamani kuua mtu.

"Gift Mushi alipigwa risasi moja ya mguu, mbili za tumboni baada ya kumuona anaendelea kuangaika chini alienda kummalizia kwa kumpiga risasi  tatu kichwani na baadaye kurudi kwenye kiti alichokaa kujimalizia mwenyewe kwa kujipiga risasi moja kichwani," amesema Karim Hussen.

"Alikuja toka asubuhi akiwa na gari yake ambayo alimpa ufunguo aitengeneze huku mwenyewe akiwa anaendelea kunywa na kuwatisha wenzake muda wote na baadae Gift Mushi ambaye ni marehemu akamfuata kumshauri aache kuwatisha wenzake wakati wakinywa."

"Baadaye kuna jamaa mmoja alikuwa anakunywa  naye silijui jina lake akamuambia kwamba kuwa yeye ni usalama wa taifa na kumuonesha kitambulisho baadae alitulia na kuanza kuomba msamaha, alikaa kimya kwa muda akawa anajishauri ghafla alitoka kwenye kiti alichokaa na kwenda hadi kwa DJ kumuambia azime muziki nako alikataliwa" amesema Lema.

Lema amesema "Kossoro baada ya kukataliwa kuzima muziki alianza kuongea kwa sauti kubwa na kusema  watu katika baa wanajifanya usalama na kuchomoa bunduki yake kuanza kupiga risasi juu baadae Gift Mushi alipomfuata kumshauri alipigwa risasi ya mguu kabla ya hajakaa sawa alipigwa risasi mbili za tumboni  na akuanguka chini  na watu wengine walikuwa wanakunywa walianza kukimbia," amesema.

Amesema wakati huo Gift Mushi alikuwa chini anahangaika baadae alimfuata tena kumpiga risasi tatu kumalizia kumuua na baadae alitoka nje ya baa na kwenda kwenye gari yake kufungua mlango alikuta umefungwa.

Husseni anaeleza "baada ya kuona mlango haufunguki alirudi tena kwenye baa na kukaa kwenye siti yake kisha kujipiga risasi ya kichwa na baadae sisi tulijitokeza,"

Husseni amesema siku hiyo Gift Mushi hakulewa isipokuwa Alex Korosso alikuwa amekuwa na tabia ya kuwatisha watu kwenye baa hii toka miezi miwili alipoanza kumiliki silaha hiyo yenye magazini 16," amesema.

 

Credit:MwananchiDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post