ASHTUKA BAADA YA KUBAINI ANAISHI NA FAMILIA YA NYOKA CHINI YA KITANDA CHAKE CHUMBANI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, July 18, 2021

ASHTUKA BAADA YA KUBAINI ANAISHI NA FAMILIA YA NYOKA CHINI YA KITANDA CHAKE CHUMBANI

  Malunde       Sunday, July 18, 2021


Mfano wa nyoka

Je utahisi vipi ukigundua umekuwa ukilala na nyoka chumbani mwako? Haya yamempata mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani ambaye amepigwa na bumbuwazi baada ya kutambua amekuwa akiishi na nyoka 18 chini ya kitanda chake.

Trish Wilcher alishtuka sana alipogundua kuna familia ya nyoka hao waliokuwa wakiishi katika chumba chake cha kulala nyumbani kwake Augusta, Georgia, Marekani. 

Katika posti kwenye mtandao wa Facebook, mnamo Jumatatu, Julai 12, Trish alipakia picha ya nyoka hao akisema kuwa: “Angalia nyoka wote hawa waliopo katika chumba changu cha kulala. yaaani nimechanganyikiwa.”

Kulingana na Trish, hii ni baada ya mumewe Max kugeuza kitanda chao cha kulala juu chini kuangalia kilichotokea na kisha walishtuka kupata watoto 17 wa nyoka na mama yao. 

Trish alisema huenda nyoka hao waliingia nyumbani kwao kutokana na shughuli ya ujenzi uliokuwa unaendelea mkabala na makazi yao hivyo nyoka hao walikimbia humo kutafuta hifadhi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post