ANNA HENGA : MATATIZO YA NDOA YANASABABISHA WANAWAKE KULEA WATOTO PEKE YAO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 22, 2021

ANNA HENGA : MATATIZO YA NDOA YANASABABISHA WANAWAKE KULEA WATOTO PEKE YAO

  Malunde       Thursday, July 22, 2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga

Na Jackline Lolah Minja - Morogoro.

Katika kuendelea kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii , Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimesema kimeandaa mpango maalumu wa kulinda na kutetea haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Akifungua kikao kazi cha kupitia ubora wa mabaraza ya ndoa na sheria za uasili watotokilichofanyika mkoani Morogoro,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Anna Henga amesema matatizo ya ndoa yamekuwa ni changamoto katika jamii na kupelekea wanawake kuishia kubaki na watoto na kulea wenyewe hivyo huathiri jamii kwa ujumla.

"Watoto huathiriwa zaidi na migogoro ya ndoa kwani wengi hutelekezwa na huingia katika wimbi la vitendo vya kikatili hasa pale familia zinapovunjika na watoto wengi hukosa muongozo, hivyo idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani inaongezeka",amesema Anna Henga.

Kwa upande wake Twaha Kibarula ambaye ni  Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto amesema kikao hicho kitajalidi na kuweka utaratibu bora utakaowasaidia watoaji huduma za usuluhishi wa migogoro ya ndoa kutoka ngazi mbalimbali.

"Hapa tutajadili njia bora zaidi ya wazazi au walezi kupata vibali kisheria ili waweze kupata huduma za malezi ya kambo na kuwasili kwa kiingereza tunaita fostcare and adoption, kutokana na utendaji wa jambo hili ulikuwa hauko sawa", amesema twaha.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post