Breaking

Post Top Ad

https://refpasrasw.world/L?tag=d_1066073m_7669c_&site=1066073&ad=7669

Saturday, July 31, 2021

KATIBU MKUU WA UVCCM KENANI KIHONGOSI AWAAGIZA WENYEVITI NA MAKATIBU WA CCM KUANZISHA KLABU ZA MAZOEZI

 


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kenani Kihongosi amewaagiza Wenyeviti na makatibu wa Chama hicho kwa ngazi ya mikoa  kuanzisha utaratibu wa Club  za mazoezi kwa kila Mkoa ili kuwahamasisha vijana kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Vijana Joging Club uliofanyika kwa lengo la  kuwapa fursa vijana kuwa na utayari wa kufanya mazoezi mara kwa mara kuepukana na maradhi hasa ya Corona.

Akiongea kwenye uzinduzi huo Kihongosi amesema Jumuiya hiyo imezindua program hiyo ambayo itawahusu vijana kwa nchi nzima na sio Dodoma peke yake huku ikiongozwa na kauli mbiu ya"amani yetu,maisha yetu".

"Fanyeni mazoezi mjikinge na magonjwa,hasa katika kipindi hiki ambapo dunia inapambana na corona,"amesema.

Mbali na hayo Katibu huyo pia ametumia nafasi hiyo kuwashawishi watanzania hususani vijana,kuona umuhimu wa kuungana na Serikali Katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona  kwa kukubali kupokea chanjo ya ugonjwa huo ambayo tayari imeshaingia nchini.

"Sisi kama vijana tunampongeza Mama yetu Samia kuleta suala la chanjo kwenye nchi yetu kwani linatuhakikishia usalama wa afya zetu hivyo ni wajibu wetu kujitokeza na kuepuka kusikil8za watu wanaopotosha,"amesisitiza.

Kupitia uzinduzi huo Katibu huyo wa jumuiya ya Vijana wa CCM amefikisha ujumbe pia kwa watanzania kuepukana na maneno ya kuyumbishwa kwani yanaweza kuvuruga amani ya nchi .

"Nchi yetu itajengwa na sisi watanzania,kumbukeni amani yetu ndiyo  maisha yetu,amani ikitoweka ni sisi tunaotaabika,"amesema.

Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewahakikishia kuwapa ushirikiano  vijana kwenye masuala ya michezo.

"Michezo ni ajira,ni matumaini yangu jumuiya hii ya UVCCM itaendelea kuwaandaa vijana ,nami naahidi kushirikiana na Katibu wa UVCCM kuunga mkono juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan  tukiwa  bega kwa bega kuhakikisha vijana wetu wanakuwa mstari wa mbele Katika kutetea na kulinda afya zao,"amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Bill Chidabwa ameeleza kuwa michezo ni fursa  kwa  vijana kwani huwakutanisha, kuwaunganisha na kuwapa ajira.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages