BIBI AFARIKI DUNIA KWENYE FOLENI AKISUBIRI FEDHA ZA KAYA MASKINI 'INUA JAMII'



Ajuza mwenye umri wa miaka 77 amefariki dunia wakati akisubiri kupokea msaada wa fedha za Mradi wa serikali wa 'Inua Jamii'.

Martha Ondieng’a kutoka kijiji cha Bwonare Kusini Mugirango, Kaunti ya Kisii  nchini Kenya alikuwa amewasili katika Ofisi ya Naibu Kamishna wa Kaunti katika eneo la Etago akitarajia kupokea msaada huo  Alhamisi, Julai 22,2021.

 Kulingana na mashuhuda, ajuza huyo alikuwa kwenye foleni akingojea zamu yake ya kupokea pesa wakati aliomba kuketi chini kutulia baadaya kulalamika kuhisi uchovu.

 Aliondoka kwenye foleni na kwenda kupumzika chini ya kivuli.

 Waliokuwepo kwenye foleni walidhani kwamba alikuwa amebebwa na usingizi mzito lakini baadaye walipatwa na mshtuko kugundua kwamba alikuwa bibi huyo amekata roho.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha Etago walifika eneo la tukio na kupeleka mwili kwenye makafani ya Hospitali ya Tabaka wakisubiri kufanyika kwa upasuaji ili ibainike kilichomuua.

 Mapema mwezi huu, serikali ya Kenya ilitoa Ksh.8.7 bilioni za malipo kwa waliosajiliwa chini ya Programu ya Inua Jamii. Hela hizo zilinuia kuwasaidia watu walio katika mazingira magumu ya umaskini na vile vile njaa.

 Nelson Marwa, Katibu wa Kudumua katika Idara ya Masuala ya Ulinzi wa Jamii alisema malipo hayo yatatumwa kwenye akaunti za walengwa waliosajiliwa kihalali kuanzia Jumatatu, Julai 12.

 Kulingana na katibu huyo wa kudumu wanaopaswa kufaidika na pesa hizo watapokea KSh 8,000 ambapo ni malipo ya miezi ya Machi, Aprili na Juni 2021.

CHANZO -TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments