Tanzia : ALIYEWAHI KUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ALLY NASSORO RUFUNGA AFARIKI DUNIA

Ally Nassoro Rufunga enzi za uhai wake

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga amefariki dunia leo Jumapili Julai 18,2021.

Taarifa za chanzo cha kifo chake bado hazijajulikana na mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)  katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Ally Nassoro Rufunga alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2016.

R.I.P Rufunga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post