JAMAA AFARIKI GESTI...POLISI WASEMA ALIMEZA VIDONGE VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME KUPITA KIASI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, July 29, 2021

JAMAA AFARIKI GESTI...POLISI WASEMA ALIMEZA VIDONGE VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME KUPITA KIASI

  Malunde       Thursday, July 29, 2021
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Fredrick Opiyo mwenye umri wa miaka 50 amefariki dunia kwa njia tatanishi kwenye lojini (Guest house) ya Rurago kaunti ya Muranga nchini Kenya.

Kulingana na ripoti ya polisi, huenda jamaa huyo alimeza vidonge vya kuongeza nguvu za kiume kupita kiasi.

Mlinzi wa lojini hiyo alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Maragua baada ya mpenzi wa jamaa huyo waliyekuwa naye kumfahamisha kuhusu kifo cha mwanaume aliyekuwa naye chumbani.

Mary Mwende alisema mpenzi wake Fredrick Opiyo alikuwa amekodi chumba cha kulala mwendo wa saa tatu usiku, naye alijiunga naye mwendo wa saa nne siku ya Jumatatu, Julai 26,2021.

Kabla ya wawili hao kulala, Mwende alisema walienda kutafuta chakula cha jioni, walikula ugali kwa samaki na mpenzi wake hakuonyesha dalili za kuwa mgonjwa.

"Jamaa huyo baadaye aliingia kwenye bafu akaoga, alimweleza mpenzi wake waingie kitandani walale lakini naye alitaka kuoga. Alipoondoka kwenye bafu, alimkuta marehemu akiwa amelala kwenye kitanda akiwa na matatizo ya kupumua, dakika chache baadaye alikata roho," Ripoti ya polisi ilieleza.

Polisi walipata mipira tatu ya kondomu, moja ikiwa imetumika na miligramu 100 ya viagra ( dawa za kuongeza nguvu za kiume) kwenye chumba hicho.

Afisa mkuu wa Muranga Kusini alifika eneo la tukio na mwili wa marehemu kusafirishwa hadi makafani ya hospitali ya Murang'a Level 5 ambapo umehifadhiwa.

Hata hivyo, uchunguzi zaidi unafanya kubaini hasa chanzo cha kifo chake.

 Chanzo - Tuko News
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post