MKUU WA MKOA WA MWANZA APIGA MARUFUKU MIKUSANYIKO

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel amepiga marufuku mikusanyiko yote isiyo ya lazima kama njia ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

“Mkoa wetu, hasa jiji la Mwanza ni Hub (kitovu) cha mikusanyiko ya watu kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na nchini jirani ambako kuna kasi kubwa ya maambukizi ya corona,”amesema Gabriel.

Huku akionyesha msisitizo, kiongozi huyo amesema; “Viongozi lazima kufanya kila linalowezekana kulinda watu; ni bahati mbaya wengi bado hawazingatii kanuni za afya za kujikinga kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa majitiririka, kutakasa mikono kwa kwa kutumia vipukusi na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima".

Via Mwananchi

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments