MAHAKAMA YAAMURU MIILI YA WATU 61 WASIOJULIKAN IZIKWE HARAKA IWEZEKANAVYO

Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru miili 61 ya watu wasiotambulika katika mochwari mbali mbali za hospitali za kaunti ya Kisumu zizikwe haraka iwezekanavyo.

Afisa mkuu wa afya kaunti hiyo Fredrick Olouch ameambia vyombo vya habari kwamba miili hiyo imezikwa katika makaburi ya pamoja katika makaburi mbali mbali ya umma kaunti hiyo. 

Oluoch pia alisema kuna miili mingine 16 ambayo itazikwa endapo familia hazitajitokeza kuwatambua jamaa zao kwa kipindi cha wiki moja.

Afisa huyo alisema kati ya miili hiyo ambayo haijatambulika, 13 imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Kisumu na mingine katika hospitali tofauti katika kata ndogo ya Ahero.

Oluach alisema notisi ilikuwa imetolewa kwa umma lakini familia hazijafika kuchukua miili ya jamaa zao na sasa kilichosalia ni kuizika ili kupunguza msongamano kwenye mochwari. 

Serikali awali ilikuwa imeagiza hospitali kutohifadhi miili kwa zaidi ya saa 48 ikiwa ni mojawapo wa masharti yaliowekwa ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya COVID-19. 

Vifo vingi vinazidi kurekodiwa nchini kutokana na maambukizi ya virusi hivyo, kufikia sasa visa vya maambukizi vilivyorekodiwa nchini ni 193,189 na sampo zilizopimwa ni 2,059,193.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments