MWANAMKE AKUTWA MTUPU , AMEUAWA SHINYANGA MJINIAskari wa Jeshi la Polisi wakichukua mwili wa Marehemu Lucia Michael.

Na Marco Maduhu, Shinyanga

Mwanamke Lucia Michael maarufu Mama Kulwa, mkazi wa Majengo Manispaa ya Shinyanga, amekutwa ameuwa na watu wasiojulikana, na mwili wake kutupwa nyuma ya msikiti wa Majengo ukiwa hauna nguo 'mtupu'.

Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo aligundulika na majirani majira ya saa 12 asubuhi  mara baada ya kuuona mwili wake ukiwa nyuma ya msikiti wa Majengo jirani na makazi yao akiwa mtupu.

Akielezea tukio hilo mmoja wa majirani Anastazia Amos, alisema baada ya kupata taarifa, alifika eneo la tukio na kumkuta jirani yake akiwa mtupu huku ameuawa, ndipo wakamfunika nguo na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa mtaa.

"Mwanamke huyu ni jirani yetu ana watoto watatu, na kazi yake ni msusi maarufu sana hapa mtaani kwetu, tunasikitika sana kumkuta akiwa ameuawa tena kavuliwa nguo zote," alisema Amosi.

Naye Mwenyekiti wa Majengo Manispaa ya Shinyanga Iddi Bwana, alisema mwanamke huyo huenda aliuawa na vibaka, na kisha mwili wake kutupwa nyuma ya Msikiti jirani na makazi ya watu.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kubainisha kuwa Jeshi bado linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo chake na wahusika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post