Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa, akiwa katika Stendi ya Mabasi ya kwenda wilayani, amewataka wananchi wa Shinyanga kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo wa Corona, kwa kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka, kuvaa barakoa, kupaka vitakasa mikono, pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile, aliwataka wananchi pale wanaposikia dalili za ugonjwa huo, wawahi kwenye huduma za afya, huku akitaja vituo ambavyo vimetengwa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo, kuwa ni Hospitali ya Rufaa, Kolandoto, kituo cha afya Kambarage.
Aidha Dk. Ndungile alitaja vituo vingine kuwa ni Kituo cha afya Tinde, Bugarama, Nyamilangano, Hospitali ya Iselamagazi wilayani Shinyanga pamoja na Hospitali ya wilaya ya Kahama, huku akitaja dalili za ugonjwa huo kuwa ni kuchoka, kusikia homa, viungo kuuma, kushindwa kupumua vizuri, na kuharisha.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Philemon Sengati, akizungumza katika Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga na kuwataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kuchukua Tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndugile, akielezea dalili za ugonjwa wa Corona wimbi la Tatu, huku akibainisha vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Corona.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Luzila John, akielezea hali ya wagonjwa wa Corona Hospitalini hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, akiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona katika Stendi ya Mabasi.
Elimu ya kujikinga na Corona ikiendelea kutolewa.
Elimu ya kujikinga na Corona ikiendelea kutolewa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Philemon Sengati akiendelea kutoa elimu ya kujinga na Corona katika Stendi ya Mabasi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk, Philemon Sengati, akinawa mikono ya majitiririka katika Stand ya Mabasi alipowasili kutoa elimu ya kujikinga na Corona.
Awali watumishi wa Serikali mkoani Shinyanga wakitakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona maofisini mwao.
Awali watumishi wa Serikali mkoani Shinyanga wakitakiwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona maofisini mwao.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Philemon Sengati, kushotom akiwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk, Luzila John, alipowasilia kuwajulia hali wagonjwa wa Corona.
Na Marco Maduhu Shinyanga.
No comments:
Post a Comment