POLISI ALIYEUA WANAUME WAWILI ADAIWA KUJIUA KWA KUJIPIGA RISASI



Afisa mmoja wa polisi ambaye amekuwa mafichoni baada ya kuwaua watu wawili amepatikana ameaga dunia.

Mwili wa Caroline Kagongo ambaye amekuwa akisakwa baada ya kuwaua watu wawili,umepatikana nyumbani kwa wazazi wake kaunti ya Elgeyo Marakwet eneo la Rift Valley.

Kulingana na polisi afisa huyo alimpiga risasi mwenzake John Ogweno Jumatatu tarehe 5 Julai na kisha kutorokea eneo la Juja viungani mwa mji wa Nairobi alipomuua mwanaume mwingine aliyetambuliwa kama Peter Ndwiga kwa kumpiga risasi katika chumba cha malazi hotelini.

Vyombo vya habari nchini Kenya vinamnukuu Kamishna wa Kanda ya Rift Valley George Natembeya kuthibitisha kisa hicho.

Ripoti hizo zinasema Kagongo alijiua kwa kujipiga risasi kutumia bastola ambayo alikuwa amejihami nayo na anayoshukiwa kuitumia kutekeleza mauaji ya hapo awali.

Mwili wake ulipatikana bafuni ambako alijiua mwendo wa saa moja unusu asubuhi.

Kagongo amekuwa akisakwa na polisi kwa wiki mbili .

Alikuwa amejihami

Polisi wamekuwa na wakati mgumu kujua aliko kwa sababu aliiacha simu yake katika eneo la kwanza alikotekeleza mauaji .

Mkurugenzi wa idara Jinai George Kinoti alitoa wito kwa umma kuwasaidia kumkamata polisi huyo ambaye alimtaja kuwa "Sugu, aliyejihami na hatari".

Kangogo amehudumu katika vituo mbalimbali vya polisi, pamoja na kitengo cha polisi wa Reli, kabla ya kupelekwa Nakuru, ambapo amekuwa akifanya kazi kwa karibu miaka mitatu.

."Tunaonya wananchi , haswa wanaume, kuchukua tahadhari dhidi ya afisa huyo mwovu ambaye anawashawishi wanaume katika mtego wake kabla ya kuwaua kikatili," alisema.

CHANZO - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments